Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2021

KUJIKUBALI

T ujikubali Ni hatua muhimu Katika maisha ambayo Kila mtu mwenye kutamani kuwa mtu fulani angepaswa kuwa nayo. Nakubali kuwa si kitu rahisi kwa sababu hupwekesha sana hasa inapotokea hakuna mtu anayekuunga mkono Katika njia hiyo ngumu yenye miiba na ya kipekee. Lakini bado unapaswa kujikubali na kutetea hoja zako za msingi kivitendo ukiidhihirishia dunia kuwa unamaanisha lakini sio Maneno matupu. Nani anajua utakuwa Nani Badae?! Nani atakayekusimamia? Lakini ukiacha utajilaumu maisha kw maisha na Wala hutokuja jisamehe kwa kushindwa kwako kulisimamia. Matajiri wengi wakubwa duniani hasa wale walioanzia hatua ngumu ya Kwanza ya utafutaji wa kuchosha na kukatisha tamaa walisaidiwa na misukumo ya mioyo yao iliyojikubali na kuwapa misisimuko kila walipopiga hatua bila kuchoka na hatimaye leo Ni watu wakubwa wa mfano kwa mfanya biashara yeyote mwenye fikra za malengo mapana zaidi, wamekuwa Ni mifano ya kuigwa. Unayo nafasi simama jitathmini itambue hadhi yako. Ishikilie na kuihefadhi maana ...